Kipindi cha Pasaka

| Mwaka wa liturujia |
|---|
| Magharibi |
| Mashariki |

Kipindi cha Pasaka ni kipindi maalumu cha mwaka wa Kanisa katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo. Kinatanguliwa na Kwaresima, kinaanza katika Dominika ya Pasaka na kukamilishwa na Pentekoste[1][2][3] au pengine Kupaa Bwana. Kinaadhimishwa kama sikukuu moja tu [4][5], ingawa siku nane za kwanza zinaunda Oktava.
Ni kwamba Wayahudi wanaadhimisha Pasaka ya kale, ukumbusho wa kuvuka pakavu kati ya bahari, kutoka utumwani kuelekea uhuru. Kumbe Wakristo wanaadhimisha Pasaka mpya, ukumbusho wa sadaka ya Agano Jipya la milele ambayo pamoja na Yesu wanavuka toka dunia hii kwenda kwa Baba: Kristo asingefufuka imani hiyo ingekuwa bure.
Maelezo yafuatayo yanatokana na mpango wa Kanisa Katoliki, lakini kwa kiasi kikubwa yanafaa pia kwa madhehebu mengine, kama vile Anglikana.
Adhimisho
[hariri | hariri chanzo]Kile cha Pasaka, kikiwa na siku hamsini, ndicho kirefu zaidi kati ya vipindi vikuu vinne vya mwaka wa Kanisa (vingine vikiwa Majilio, Noeli na Kwaresima).
Wakati wa Pasaka Agano la Kale halisomwi kwa kuwa yaliyotabiriwa nalo yameshatimia katika Kristo. Badala yake yanasomwa karibu mfululizo Matendo ya Mitume yanayoelekeza safari yote ya Kanisa. Masomo mengine, sala na nyimbo vinasema hasa juu ya Kristo kufufuka na kuwa na watu wake kwa namna mpya, pia juu ya paji la Roho Mtakatifu alilowapatia.
Katika maisha ya kawaida watu wanafanya sherehe mbalimbali, si za dini tu. Sikukuu yoyote inatokeza furaha ya kuishi: usipokuwa na mtazamo wa kuridhika na maisha, kumwaga pesa katika anasa hakuondoi huzuni ya kukata tamaa. Sikukuu yoyote ni adhimisho la pamoja: inatokana na watu kukubaliana katika kujali mambo fulanifulani au walau kuheshimiana; pia inajenga jamii kwa kurudisha furaha ya kuwa pamoja.
Kwa Wakristo sherehe kuu kuliko zote ni Pasaka: ndiyo sikukuu yenyewe ambayo inadumu siku hamsini mfululizo hadi Pentekoste na inaitwa Dominika kubwa. Kwa kweli Pasaka si sherehe mojawapo tu wala kipindi kimojawapo tu katika mwaka wa liturujia, bali ndiyo kiini chake, kama vile Dominika (Pasaka ndogo ya kila wiki) ilivyo kiini cha juma zima. Ni adhimisho la uzima mpya na wa milele ambao Kristo mfufuka anaushirikisha kwa njia ya sakramenti: ubatizo na kipaimara kwa Wakristo wachanga, kitubio kwa waliobatizwa zamani, hasa ekaristi kwa wote; humo Yesu hakumbukwi tu, bali waaminu wanakutana naye, hai tena mtukufu. Adhimisho hilo ni la pamoja kwa sababu wamekuwa moyo mmoja na roho moja katika Kristo kwa kumiminiwa Roho Mtakatifu. Kwa kumega mkate mmoja wanaimarisha ushirika wao na kuwajibika kumtambua Yesu katika wale wote wanaokutana nao, hasa maskini.
Mang’amuzi hayo ya imani yanachochea kuimba mfululizo Aleluya! Bila shaka inaimbwa na watu wakiwa njiani kuelekea kwao: hawajafikia pale watakapoimba katika heri ya starehe ya milele. Wanaimba wasije wakalemewa na mzigo wa maisha. Augustino wa Hippo alionya: “Imba anavyofanya msafiri. Imba lakini tembea, usahau uchovu wako kwa kuimba, lakini jihadhari na uvivu. Imba na tembea”. Aleluya inatokeza vizuri furaha na tumaini: ndiyo sababu ikaririwa sana. Pamoja na hayo, uhuru wa Kikristo unawadai waamini wAUshuhudie kwa matendo na hasa kwa kuwakomboa ndugu zao wanaodhulumiwa.
Kristo amefufuka kweli na atawafufua wote pia: waamini wake wataishi naye kwa Baba katika umoja wa Roho Mtakatifu. Hata sasa yu pamoja nao (ndiyo maana ya mshumaa wa Pasaka). Wakiwa naye maisha yanawanogea, kwa kuwa yote yameinuliwa tena na kufanywa mapya. Wanaamini wamekombolewa kutoka utumwa wa dhambi na mauti, wamekuwa wana wa Mungu na kuishi kwa uhuru wa upendo wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Kristo amekuwa Bwana na anaendelea kueneza ufalme wake. Hawawezi kuogopa chochote tena kwa kuwa historia ni yake yeye aliye Alfa na Omega.
Nje ya liturujia
[hariri | hariri chanzo]Katika utamaduni wa Kikristo kipindi cha Pasaka kina desturi mbalimbali kadiri ya madhehebu na nchi, kama vile mapambo [6][7][8][9][10][11], na hasa upande wa chakula, kwa mfano mayai ya Pasaka [12][13][14][15][16].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Normae Universales de Anno Liturgico et de Calendario (NUALC), 22
- ↑ "Saints Will Arise: So which Sunday in Eastertide is it? Take your pick!" (kwa Kiingereza). Saints Will Arise. 13 Aprili 2013. Iliwekwa mnamo 2 Mei 2019.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ NUALC, 23
- ↑ Saint Athanasius, Epist. fest. I: Patrologia Graeca 26, 1366
- ↑ "Ascension Day: Ascension of Our Lord".
- ↑ "The Flowering of the Cross" (kwa English). First Global Methodist Church of Forney. 19 Machi 2021. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Aprili 2023. Iliwekwa mnamo 10 Aprili 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ Friedman, Sally (27 Machi 2016). "Easter bonnets top at Burlington City shop" (kwa English). Burlington County Times. Iliwekwa mnamo 10 Aprili 2023.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ Simpson, Jacqueline; Roud, Steve (2003). "clipping the church". Oxford Reference. Oxford University Press. doi:10.1093/acref/9780198607663.001.0001. ISBN 9780198607663. Iliwekwa mnamo 30 Machi 2013.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Collins, Cynthia (19 Aprili 2014). "Easter Lily Tradition and History". The Guardian. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 20 Aprili 2014.
The Easter Lily is symbolic of the resurrection of Jesus Christ. Churches of all denominations, large and small, are filled with floral arrangements of these white flowers with their trumpet-like shape on Easter morning.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Schell, Stanley (1916). Easter Celebrations. Werner & Company. uk. 84.
We associate the lily with Easter, as pre-eminently the symbol of the Resurrection.
- ↑ Luther League Review: 1936–1937. Luther League of America. 1936. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 20 Juni 2015.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Anne Jordan (5 Aprili 2000). Christianity. Nelson Thornes.
Easter eggs are used as a Christian symbol to represent the empty tomb. The outside of the egg looks dead but inside there is new life, which is going to break out... Orthodox Christians dye boiled eggs red to make red Easter eggs that represent the blood of Christ shed for the sins of the world.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ The Guardian, Volume 29. H. Harbaugh. 1878.
Just so, on that first Easter morning, Jesus came to life and walked out of the tomb, and left it, as it were, an empty shell. Just so, too, when the Christian dies, the body is left in the grave, an empty shell, but the soul takes wings and flies away to be with God. Thus you see that though an egg seems to be as dead as a stone, yet it really has life in it; and also it is like Christ's dead body, which was raised to life again. This is the reason we use eggs on Easter.
- ↑ Gordon Geddes, Jane Griffiths (22 Januari 2002). Christian belief and practice. Heinemann. ISBN 9780435306915.
Red eggs are given to Orthodox Christians after the Easter Liturgy. They crack their eggs against each other's. The cracking of the eggs symbolizes a wish to break away from the bonds of sin and misery and enter the new life issuing from Christ's resurrection.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Vicki K. Black (1 Julai 2004). The Church Standard, Volume 74. Church Publishing, Inc. ISBN 9780819225757.
In parts of Europe, the eggs were dyed red and were then cracked together when people exchanged Easter greetings. Many congregations today continue to have Easter egg hunts for the children after the services on Easter Day.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Davis, David (20 Aprili 2014). "Easter Traditions Explained". CBS News. Iliwekwa mnamo 20 Aprili 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Easter Season Resource Library – Crossroads Initiative Archived 2012-10-11 at the Wayback Machine
- Normae Universales de Anno Liturgico et de Calendario Archived 2017-04-15 at the Wayback Machine
- Writings on Easter, Eastertide and Lent liturgical days
- Liturgy of Hours of Eastertide
- Eastertide: How It's Celebrated in the Americas and Across Europe
- French translation Ilihifadhiwa 15 Machi 2005 kwenye Wayback Machine.
| Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kipindi cha Pasaka kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |

